MBINU ZA KUPUNGUZA KUKOPWA KATIKA BIASHARA
MBINU ZA KUPUNGUZA KUKOPWA KATIKA BIASHARA-01 Na Hussein Hussein Jioni moja nilipita sehemu moja ambapo yalikuwapo maduka mawili yaliyokaribiana, katikati ya maduka hayo nilikutana na wadada wawili, mmoja alimwambia mwenzake "usiende tena kununua hapo, jana nilimvyomnunuza nilipungukiwa na mia, nikmuomba anipe tu nitamletea kesho ila kaniwekea uso wa mbuzi eti hakopeshi, yani hakujali mimi mteja wake wakila siku, twende tukanunue pale hapo sinunui tena" Alimuelekea dada huyo mwenzake kwa kidole duka jingine na wakaenda hapo... twende wote Ikiwa kuna jambo hawalipendi wafanya biashara wengi basi ni kukopwa na ikiwa kuna jambo linaua na litaendelea kuua biashara basi ni kukopesha. Na ilivyo nikuwa huwezi kwepa kukopwa, wenyewe wafanya biashara wana kwambia kukopwa ndio biashara yenyewe hakuna biashara bila kukopwa. La msingi ikiwa utalazimika kukopesha basi mkopeshe mteja anaekopesheka-muaminifu na kiasi kinachokopesheka, kwa maana usikopeshe kiasi kikubwa hata kikavuruga mah...