Posts

Shairi Hisani ya kizandiki

 HISANI YA KIZANDIKI.  Tukadhani marafiki, wa kwenye jua na mvua  Kushikana kwenye dhiki, pamoja tunakenua Yote haya kumbe feki, tulichelewa kujua  WATUGAWIA SAMAKI, SIKUTUFUNZA KUVUA Kugawa wanaafiki, chewa, sato na kibua Kutufunza hawataki, eti tunawasumbua Hawa hawaaminiki, siku watatuzingua WATUGAWIA SAMAKI, SIKUTUFUNZA KUVUA Hisani ya kizandiki, sasa tumeshatambua Katu hawafurahiki, kupiga kwetu hatua Zimefichikana chuki, ndani ya vyao vifua WATUGAWIA SAMAKI, SIKUTUFUNZA KUVUA  Tumeshapiga mswaki, kisha tukasukutua Hamna taediriki, fungu lao  kuchukua Hata hatutikisiki, tumeshakwisha amua WATUGAWIA SAMAKI,   SIKUTUFUNZA KUVUA Waacheni wadhihaki, waseme moto wa bua Tuna mipango lukuki, kichumi kujikwamua Watakuja kuhamaki, nyavu tunavyonunua WATUGAWIA SAMAKI,  SIKUTUFUNZA KUVUA  Tuunge kile na hiki, tutengeneze mashua Si kazi kutamalaki, mkono aloinua Mola tupe taufiki, mipango iwe murua WATUGAWIA SAMAKI,  SIKUTUFUNZA KUVUA...

MBINU ZA KUPUNGUZA KUKOPWA KATIKA BIASHARA

 MBINU ZA KUPUNGUZA KUKOPWA KATIKA BIASHARA-01 Na Hussein Hussein Jioni moja nilipita sehemu moja ambapo yalikuwapo maduka mawili yaliyokaribiana, katikati ya maduka hayo nilikutana na wadada wawili, mmoja alimwambia mwenzake "usiende tena kununua hapo, jana nilimvyomnunuza nilipungukiwa na mia, nikmuomba anipe tu nitamletea kesho ila kaniwekea uso wa mbuzi eti hakopeshi, yani hakujali mimi mteja wake wakila siku, twende tukanunue pale hapo sinunui tena" Alimuelekea dada huyo mwenzake kwa kidole duka jingine na wakaenda hapo...  twende wote Ikiwa kuna jambo hawalipendi wafanya biashara wengi basi ni kukopwa na ikiwa kuna jambo linaua na litaendelea kuua biashara basi ni kukopesha. Na ilivyo nikuwa huwezi kwepa kukopwa, wenyewe wafanya biashara wana kwambia kukopwa ndio biashara yenyewe hakuna biashara bila kukopwa. La msingi ikiwa utalazimika kukopesha basi mkopeshe mteja anaekopesheka-muaminifu na kiasi kinachokopesheka, kwa maana usikopeshe kiasi kikubwa hata kikavuruga mah...

Shairi

 UKWELI Ukweli jama useme, tusikie wanadamu Ukweli usitunyime, tunataka kufahamu Ukweli nausimame, uongo hauna zamu Hata kama ni mchungu, ukweli utakalamu Ukweli kote uvume, Mbeya, Tanga hadi Lamu Ukweli ukawe sime, ya kukata udhalimu Ukweli ukawachome, wote wasojiheshimu Hata kama ni mchungu, ukweli utakalamu Ukweli kama umeme, kwa banati na ghulamu Ukweli usiuzime, twauhitaji kaumu Ukweli bwana Mtume, kasema jambo adhimu Hata kama ni mchungu, ukweli utakalamu Ukweli usiuhame, kwenye wakati mgumu Ukweli kwa mfalme, utaitwa mnajimu Ukweli siumeume, kwa kuhofia mabomu Hata kama ni mchungu, ukweli utakalamu Ukweli ndani ya gome, chungwa likaitwa ndimu Ukweli kwanza upime, utaona umuhimu Ukweli kama kipome, ule haishi hamu Hata kama ni mchungu, ukweli utakalamu  Ukweli wake waume, siku hizi ni chandimu Ukweli wa paka shume, unakuja kwa msimu Ukweli huwa kinyume, visipokwepo vitamu Hata kama ni mchungu, ukweli utakalamu Ukweli sote tuseme, waungwana wasalamu Ukweli hapa nikome, na...