MBINU ZA KUPUNGUZA KUKOPWA KATIKA BIASHARA

 MBINU ZA KUPUNGUZA KUKOPWA KATIKA BIASHARA-01

Na Hussein Hussein

Jioni moja nilipita sehemu moja ambapo yalikuwapo maduka mawili yaliyokaribiana, katikati ya maduka hayo nilikutana na wadada wawili, mmoja alimwambia mwenzake "usiende tena kununua hapo, jana nilimvyomnunuza nilipungukiwa na mia, nikmuomba anipe tu nitamletea kesho ila kaniwekea uso wa mbuzi eti hakopeshi, yani hakujali mimi mteja wake wakila siku, twende tukanunue pale hapo sinunui tena" Alimuelekea dada huyo mwenzake kwa kidole duka jingine na wakaenda hapo... 

twende wote

Ikiwa kuna jambo hawalipendi wafanya biashara wengi basi ni kukopwa na ikiwa kuna jambo linaua na litaendelea kuua biashara basi ni kukopesha. Na ilivyo nikuwa huwezi kwepa kukopwa, wenyewe wafanya biashara wana kwambia kukopwa ndio biashara yenyewe hakuna biashara bila kukopwa. La msingi ikiwa utalazimika kukopesha basi mkopeshe mteja anaekopesheka-muaminifu na kiasi kinachokopesheka, kwa maana usikopeshe kiasi kikubwa hata kikavuruga mahesabu na biashara yako

Ikiwa kukutaa kukopa kunafukuza baadhi ya wateja na kukopesha sana kunafukuza na kunaua biashara. Basi Leo nimekuletea mbinu tatu za kupunguza kukopwa pasipo kumfukuza mteja

-Moja, Tengeza list feki ya wateja waliokopa siku hiyo.

Badala ya kumjibu mteja mkopaji kwa kauli za kigai gai kama kumwambia mkopo ameenda likizo, Basi unaweza tumia list hii kuepuka kukopwa, mwambie mkopaji "natambua na kuthamini mchango wako ofisini kwetu kwani umekuwa ukitununuza mara nyingi, pole leo mambo yako ni magumu, na bahati mbaya kwetu leo biashara yetu ni ngumu sana na nimekopwa na watu wengi. Tizama mikopo ya siku ya leo tu, hapo siongelei jana na juzi(huku ukimuonesha majina yale feki). labda uje kesho kwa leo ni ngumu ndugu yangu." Uhakika wa mambo ni kuwa hawezi kuja kesho kwa ajili ya kukopa eti kwa kuwa jana alimwambia utamkopesha. Kesho atakuja kununua moja kwa moja, na pengine aliahidi kesho angapata pesa, hivyo ataona haya kuja bila pesa

-Ya pili, Waaminishe wateja wajue kwamba wewe ni muuzaji tu, biashara sio yako.

Katika makosa wanayofanya wafanya biashara, hasa wadogo wadogo ni kumwambia mteja hukopeshi kwa kuwa wakopaji hukimbia na kubadili sio maduka tu bali njia na makazi mara baada ya kukopeshwa. Kamwe hupaswi kumuonesha mteja kuwa humuamini. Ukionesha kutokumwamini mteja utampoteza moja kwa moja. mkopaji mwambie "asante kwa kununua kwetu, ila pole kwa kukuambia kwamba mimi sina mamlaka ya kukopesha. Ningesema nikudhamini nikukopesha ila ni juzi tu nilijitia matatizoni kwa boss wangu baada ya kufanya hivyo. Labda uje mara nyingine kama utamkuta mwenyewe ndio atakukopesha". Hii mbinu itakusaidia hata siku za mbele.

-Ya tatu, Waambie mteja mkopaji unafanya biashara ya mali kauli.

Mali kauli bi maana bidhaa ulizo nazo sio zako niza za mtu mwingine, wewe ulipewa tu uuze, kisha ukishauza unampelekea mauzo uliyopata aliyekukopa, na wewe unapata gawio au faida ya kile ulicho uza na kupewa bidhaa nyingine ukaendelee kuuza. Kwa maana nyingine mali kauli ni aina ya nyingine ya mkopo. Kwa mteja mkopaji basi muambie "ndugu yangu kwanza nashukuru kwa kuja dukani kwetu. Ndugu yangu unajua biashara yetu ni ya mali kauli na mwenye mali au bidhaa hizi anahitaji pesa zake sasa, kukopesha kutanitia matatizoni labda muda mwingine tukiwa imara nitakukopesha leo kumradhi" hii nayo ni mbinu itakayokusaidia hata huko mbeleni

Comments